Muundo wa Mashairi katika Diwani ya Mnyampala (1965) na Nafasi yake katika Kuibua Maudhui

  • Anna Nicholaus Kyamba

Abstract

Makala hii inachambua muundo wa mashairi katika Diwani ya Mnyampala (1965) na nafasi yake katika kuibua maudhui. Lengo ni kuangalia vipengele vya muundo vinavyojitokeza katika diwani hii. Vipengele vilivyoshughulikiwa ni mishororo, beti, mizani, vina, kituo au kibwagizo na mkarara. Pia, tunaangalia muundo huo ulivyotumika kuibua dhamira mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi katika diwani hiyo. Makala hii pia inadadisi namna mbinu za kimuundo zilivyofanikisha usawiri na ubainishaji wa falsafa ya mtunzi kuhusu ushairi wa Kiswahili na nafasi ya ushairi katika jamii. Makala imeanza kwa kugusia usuli wa historia ya ushairi wa Kiswahili, historia fupi ya maisha ya Mathias Mnyampala na nadharia yake kuhusu ushairi wa Kiswahili. Data za makala hii zimepatikana kwa kusoma matini husika na kuchambua vipengele vyake vya kimuundo.
Published
2017-07-27
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X