Vigezo vinavyohukumu ujumi wa utani katika familia: Uchunguzi wa familia za kizigua na kidigo

  • Hadija Kutwa Abdallah

Abstract

Makala hii imelenga kufafanua vigezo vinavyotumika kuhukumu ujumi wa utani wa familia katika jamii za Tanzania ambazo ni jamii ya Wazigua na jamii ya Wadigo. Katika ujumi tunapata kanuni, taratibu na mambo yanayohukumu uzuri au ubaya wa watu, vitu na sanaa. Kila kazi ya fasihi inatarajiwa kuwa na ujumi wake unaoendana na idili za jamii ya mtunzi na madhumuni ya mtunzi. Wataalamu kadhaa akiwamo Kagan (1975), Ameir (2011), Ponera (2014), Badru (2015) na Wamitila (2015) wamechunguza ujumi katika kazi za fasihi lakini hawakugusia hukumu ya ujumi wa utani katika familia. Hali hii inasababisha sanaa ya utani wa familia kutofahamika vema uzuri wake kiujumi kwa jamii na kuonekana kuwa ni sanaa kwa ajili ya kufurahisha na kuchekesha tu (Senyamanza, 2014). Makala hii inalenga kuondoa hali hii kwa kubainisha vigezo vinavyohukumu ujumi wa utani katika familia ya Wazigua na Wadigo ili jamii ifahamu uzuri wa kiujumi unaopatikana katika sanaa ya utani ya familia hizi. Ubainishaji ulitokana na utafiti wa uwandani uliyofanywa na mwandishi wa Makala hii. Makala hii inaongozwa na mawazo ya Nadharia ya Elimu-jamii iliyoasisiwa na Hippolyte Taine (1863). Mawazo ya Taine yamezua msingi mkuu wa nadharia hii unaoeleza kuwa fasihi ni chombo cha kuibadilisha, kuiburudisha, kuifundisha, kuirekebisha na kuiweka jamii katika mwenendo mwema (Mushengyezi, 2003). Mbinu zilizotumika kupata data za makala hii ni mbinu ya mahojiano na mbinu ya ushuhudiaji. Makala hii inatarajiwa kuwa na mchango katika uga wa fasihi simulizi kwa sababu, inalenga kuelezea vigezo ambavy, vitakuwa dira ya hukumu ya kiujumi katika utani wa familia.

Published
2021-09-07
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789