Main Article Content

Nafasi ya Shaaban Robert katika kukuza na kuendeleza Kiswahili: uchunguzi wa mashairi teule


Hassan R. Hassan

Abstract

Shaaban Robert ni mmoja wa wapenzi na waandishi maarufu wa Kiswahili. Yeye ameishi karne ya 20 na amefanya mambo mengi yenye kustawisha lugha aushi ya Kiswahili. Wataalamu mbalimbali kama Sengo (1975), Kezilahabi (1976), Gibbe (1980) na Khatib (2014) wanamtaja Shaaban Robert kama mtu aliyekuwa na nia thabiti ya kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili kupitia maandishi yake. Makala hii inachambua kwa kina kuhusu nafasi ya Shaaban Robert katika lugha ya Kiswahili kwa kuangazia fikra zilizomo katika mashairi yake teule. Kupitia fikra hizo, tumeweza kubainisha jinsi Shaaban Robert alivyokuwa mstari wa mbele katika kuikuza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili. Makala hii ni zao la uchunguzi wa kimaktaba. Mjadala unafanywa kwa kuegemezwa katika mashairi yake teule ambayo ni: “Kiswahili” kutoka Pambo la Lugha (1966), “Kila Lugha” kutoka Insha na Mashairi (1967) na “Lugha Yetu” kutoka Mwafrika Aimba (1969). Mengine ni “Kiswahili 1”, “Kiswahili 2” na “Kitakoma Kiswahili” kutoka Almasi za Afrika (1972). Makala imebaini kwamba kupitia mashairi hayo, Shaaban Robert amejitokeza katika nafasi anuwai ikiwa ni harakati zake za kukuza na kuendeleza Kiswahili. Nafasi hizo ni pamoja na mtetezi wa Kiswahili, mhamasishaji wa kukipenda Kiswahili, mwalimu wa Kiswahili na mwandishi wa vitabu vya Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789