Main Article Content

Athari za miktadha ya maisha ya jamii katika kumwibua Euphrase Kezilahabi: Uchunguzi katika <i>Rosa Mistika</i> na <i>Dunia Uwanja Wa Fujo</i>


Adria Fuluge

Abstract

Makala hii inabainisha athari za miktadha ya maisha ya jamii zinazosawiriwa katika riwaya ya Rosa Mistika (1971) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975) zilivyomwibua mwandishi wa riwaya hizo. Inafanya hivyo ili kuthibitisha kuwa fasihi ni zao la jamii na ina uwezo wa kuathiri au kuathiriwa na jamii. Athari hizo hutokana na maendeleo na mabadiliko ya jamii ambapo kadiri jamii inavyobadilika, ndivyo na mkondo wa fasihi hubadilika. Aidha, kutokana na nguvu ya kazi ya fasihi, hakuna anayeweza kubaki katika hali ileile akishaguswa na kazi ya kifasihi kwani huweza kuathiriwa katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kihisia, kiitikadi na kiutamaduni. Vilevile, kwa kuwa mtunzi pia ni zao la jamii, ni wazi kwamba mabadiliko yoyote ya kijamii yatokeapo, humwathiri kifani na kimaudhui. Kutokana na hilo, mtunzi naye hulazimika kutambua na kukubaliana na hali halisi ya maisha ya jamii yake ili iwe mwongozo wa kuzingatiwa katika utunzi wake. Data za makala hii zilipatikana kwa njia ya usomaji makini wa riwaya teule na mahojiano na watafitiwa uwandani. Uchambuzi wa data hizo uliongozwa na Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi. Hatimaye, matokeo yanaonyesha kwamba katika utunzi wake, Euphrase Kezilahabi ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na miktadha ya maisha ya jamii yake. Miktadha hiyo ambayo ni ya kijamii, kiutamaduni na kisiasa, ndiyo iliyomwibua na kumweka katika ulimwengu wa fasihi ya Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789