Main Article Content

Mdhihiriko wa falsafa ya Kiafrika katika vitendawili vya Kiswahili


Adria Fuluge
Felista Juma Ngatungwa

Abstract

Falsafa ya Kiafrika huweza kujidhihirisha kupitia vipengele mbalimbali vya maisha vinavyoakisi tajiriba za Waafrika wenyewe. Vipengele hivyo ndivyo vinavyoibua mitazamo mbalimbali ya kifalsafa inayojenga falsafa jumuifu ya Waafrika. Miongoni mwa vipengele hivyo ni vitendawili ambavyo huibua na kuipa jamii husika maarifa ya kifalsafa. Makala hii inafafanua baadhi ya vipengele vya falsafa ya Kiafrika vinavyodhihirika kupitia vitendawili vya Kiswahili. Inafanya hivyo ili kuonesha vipengele vya falsafa ya Kiafrika vinayopatikana katika fasihi simulizi ya Kiswahili, hususani katika vitendawili. Hii ni kutokana na sababu kuwa vitendawili vya Kiswahili vimebeba amali za kifalsafa, ambazo kwa kiasi kikubwa zinasaidia katika kuhifadhi maarifa ya kifalsafa ya jamii ya Waafrika kwa ujumla. Data za uchunguzi huu zilipatikana kwa njia ya udurusu wa matini mbalimbali, majadiliano ya vikundi na mahojiano uwandani. Aidha, Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi ndiyo iliyotuongoza katika kuchunguza falsafa ya Kiafrika inayopatikana katika vitendawili vya Kiswahili. Kwa ujumla, mtazamo wa nadharia hii unadai kuwa fasihi haiwezi kujitenga na jamii ambayo kwayo fasihi hiyo imechipuzwa na kukuzwa. Hivyo, nadharia hii imetuwezesha kuonesha jinsi falsafa ya Kiafrika ilivyobebwa na vitendawili vya Kiswahili. Kwa ujumla, makala imebainisha kuwa utanzu wa vitendawili una hazina kubwa katika kuhifadhi na kutunza maarifa ya falsafa ya Kiafrika, ambapo kupitia vitendawili hivyo, falsafa hizo zimedhihirika.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789