Main Article Content

Utenge wa tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili katika mabango yaliyopo Barabara Kuu ya Moshi – Arusha


Arnold B. G. Msigwa
Judith Maro

Abstract

Katika Barabara Kuu ya Moshi-Arusha, eneo la Usa River, kuna mabango anuwai ambayo yanalenga kutangaza biashara na shughuli zinazofanywa na asasi na watu binafsi. Kutokana na mwingiliano wa watu wanaotumia barabara hii, mabango haya yamelazimika kutumia uwililugha1, yaani Kiingereza na Kiswahili. Uchunguzi wa awali uliofanywa kwenye mabango mengi yaliyopo katika barabara hiyo umebaini kuwa, mbali na mambo mengine, utenge wa wazi katika tafsiri zilizomo katika mabango hayo. Hicho ndicho kilichotuchochea kufanya utafiti ulioibua makala hii. Jumla ya mabango 30 yalikusanywa kwa njia ya kupiga picha, kisha uchambuzi wa kimaudhui ulifanyika kuhusu mabango hayo. Kwa hiyo, makala hii inabainisha makosa ya tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili kwenye mabango hayo. Jumla ya mabango 30 yalitumika kama data. Kwa kuongozwa na misingi ya Nadharia ya Usawe wa Kidhima, tulibainisha dosari mbalimbali za tafsiri zilizojidhihirisha katika mabango hayo. Makosa yaliyobainishwa ni: makosa ya kisemantiki, makosa ya kimofolojia, makosa ya ki-tafsiri na makosa ya kisintaksia. Makala imehitimishwa kwa kugusia vipengele vinavyoweza kuzingatiwa ili kupunguza dosari hizo.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789