Main Article Content
Viashiria vya ufungwa wa kisaikolojia kwa wahusika katika riwaya ya kiswahili: Mifano kutoka vuta n’kuvute na kufikirika
Abstract
Makala hii imelenga kufafanua ufungwa wa kisaikolojia kwa kubainisha viashiria vyake katika riwaya teule. Nadharia iliyoongoza ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji wa data za makala hii ni Nadharia ya Saikolojiachanganuzi. Aidha, usanifu uliotumika katika makala hii ni uchunguzi kifani. Makala hii ni sehemu ya utafiti uliofanyika kwa mahitaji ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Hivyo, data zake zilipatikana maktabani kupitia utafiti uliofanywa 2023. Data za maktabani zilipatikana kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini, hususani kusoma na kuchambua riwaya teule. Matokeo yanaonesha kwamba viashiria vya ufungwa wa kisaikolojia kwa wahusika katika riwaya teule vinadhihirika kupitia vilio, manung’uniko na uteti, hali ya unyonge na kukata tamaa na kufanya matendo yasiyo ya kawaida kwa wahusika wa kazi hizo.