Main Article Content
Changamoto zinazowakabili walimu wa kiswahili katika utekelezaji wa mtaala wa Umilisi: Mfano wa shule teule za sekondari wilayani nyagatare, Rwanda
Abstract
Makala hii ina malengo mahsusi mawili: kubainisha changamoto zinazowakabili walimu wa Kiswahili katika utekelezaji wa Mtaala wa Umilisi na kubainisha mikakati na mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizo. Sampuli ya utafiti iliundwa na wanafunzi 30, walimu wa Kiswahili 3 na wakuu wa masomo 3. Hii ni kwa kuwa kila shule ina mwalimu na mkuu wa masomo mmoja tu. Eneo la utafiti lilikuwa Wilaya ya Nyagatare. Data zilipatikana kupitia ushuhudiaji, mahojiano, na udurusu wa nyaraka kutoka kwenye majarida, mtandao, tasnifu na makala mbalimbali. Data zilichanganuliwa kwa kutumia Nadharia ya Utekelezaji wa Mtaala iliyoasisiwa na Gross mwaka 1971. Kisha, ziliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Changamoto zilizobainika ni uhaba wa vifaa vya ufundishaji, uwezo mdogo wa lugha ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi, uhaba wa mafunzo walimu, mtazamo hasi wa walimu kuhusu matumizi ya TEHAMA, ukosefu wa ushirikiano kati ya walimu na wazazi, na mtazamo hasi wa walimu kuhusu Mtaala wa Umilisi. Makala hii inapendekeza uongezaji wa rasilimali za kufundishia, ushirikiano wa wakuzaji wa mtaala na wadau wengine, na utoaji wa mafunzo ya walimu kuhusu mbinu bora za ufundishaji wa Kiswahili katika mazingira ya Mtaala wa Umilisi.