Main Article Content
Utekelezaji wa mtaala unaoegemea katika uwezo kupitia fasihi : Maoni kutoka kwa walimu na wanafunzi katika shule teule za sekondari
Abstract
Makala hii inaijadili fasihi kama nyenzo mwafaka ya utekelezaji wa mtaala unaoegemea katika uwezo kutokana na stadi za karne ya 21, masuala mtambuka, na maadili na mwenendo mwema kupewa uzito katika mtaala huu. Wango la utafiti lilikuwa ni walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika kidato cha tano katika shule teule za sekondari nchini Rwanda pamoja na kazi za fasihi zinazotumiwa na walimu wakati wa ufundishaji. Sampuli ilipatikana kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa. Nadharia ya Mwingiliano wa Tamaduni-jamii iliongoza hatua mbalimbali za utafiti ulioibua haja ya kuandika makala hii. Aidha, ukusanyaji wa data ulitumia mbinu ya ushuhudiaji, uchambuzi wa matini na mahojiano. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kwamba fasihi hutoa mifano mwafaka ya uwezo wa jumla, masuala mtambuka na mitazamo na thamani. Kwa hivyo, sifa hii sio tu inaifanya fasihi kuwa nyenzo mwafaka ka ya utekelezaji wa mtaala unaoegemea katika uwezo bali pia kudhihirisha umuhimu wa nyuga za kiinsia hata katika zama za sasa.