Main Article Content
Matumizi ya msamiati katika jamiilugha ya wafanyabiashara wa soko la karume katika jiji la Dar Es Salaam
Abstract
Makala hii inalenga kubainisha msamiati maalumu wa Kiswahili unaoibuliwa na wafanyabiashara wanaouza viatu vya mtumba katika soko la Karume jijini Dar es Salaam. Aidha, inalenga kuchunguza jinsi wafanyabiashara hao wanavyoutumia msamiati huo katika mchakato mzima wa kuendesha biashara zao katika miktadha mbalimbali. Utafiti huu, ni matokeo ya data za uwandani za usaili na ushuhudiaji. Data zingine zilipatikana maktabani kupitia usomaji wa nyaraka zinazoakisi mada hii kama vile: vitabu, tasnifu pamoja na majarida mbalimbali. Mbinu zote hizo kwa pamoja zimemsaidia mtafiti kupata data faafu zinazotosha kujibu lengo la makala hii. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi wa Kimaeneo ya Fishman (1972) na data zimechanganuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Kwa ujumla, matokeo ya uchunguzi yameweka wazi msamiati fiche wa Kiswahili unaotumiwa na wafanyabiashara hao. Hivyo, tunapendekeza msamiati huo upitiwe na vyombo vilivyopewa dhamana ya kuunda istilahi, ili kuona namna bora ya kuweza kuusanifisha.